SHULE YA SEKONDARI YA MUSTLEAD iliyopo barabara ya Bagamoyo – Msata, Masuguru, Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, imeandaa shindano la uandishi wa insha kwa washiriki ambao wako chini ya taasisi rasmi mfano taasisi za elimu (shule, vyuo n.k) taasisi za kidini, fedha n.k., Asasi au Vikundi n.k. Lengo la shindano hili ni kujenga umahiri na kukuza lugha ya kiswahili nchini na kuzitambua fursa za kujiajiri.
MADA: ZIPO FURSA NYINGI ZA KUJIAJIRI TANZANIA
MAMBO MUHIMU: Washiriki wawe na umri kati ya miaka 15 hadi 30. Insha iandikwe kwa lugha ya kiswahili. Anuani na namba ya simu ya mshiriki kupitia taasisi, asasi au kikundi chake ioneshwe kwa usahihi. Insha iwe na maneno yasiyopungua 800 na yasiyozidi 1000, na iandikwe kwa mkono. Mshiriki awe chini ya taasisi, asasi au kikundi. Ambapo watakaa na kukubaliana insha moja watakayo iwasilisha, yenye jina la mwakilishi wa taasisi, asasi au kikundi hicho. Vigezo vya uandishi wa insha vizingatiwe.
ZAWADI: Mshindi wa kwanza TSH 300,000 pamoja na Tshirts na Vitabu vya Ujasiriamali; Mshindi wa Pili TSH 200,000 pamoja na Tshirt na Vitabu vya Ujasiriamali; na Mshindi wa Tatu TSH 100,000 pamoja na Tshirt na Vitabu vya Ujasiriamali. Mshindi 4 hadi 10 watapatiwa Tshirt na Vitabu vya Ujasiriamali n.k. Aidha, Washiriki wote watapata fursa ya kutambuliwa na kuingizwa kwenye orodha ya wabia wa ushirikiano wa shule ya Sekondari ya MUST LEAD na taasisi zake.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Insha zote zitumwe kwa njia ya posta, usitumie barua pepe. Juu ya bahasha andika:
MUSTLEAD SECONDARY SCHOOL SHINDANO LA INSHA S.L.P 211 BAGAMOYO, PWANI AU 25247 ILALA, DAR ES SALAAM
Unaweza pia kuleta ofisini mapokezi moja kwa moja, saa za kazi (saa 2:00 asubuhi hadi 11:00 jioni). Mwisho wa kupokea insha zote ni tarehe 20 – 05- 2022. Washindi watatangazwa mwezi wa sita, 2022.
Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana na Mratibu wa Shindano Madam Janeth Mbuya simu 0713 150 841 au Mratibu Msaidizi Mwl. Fatuma Swedy simu 0687 559 343.
Kauli mbiu yetu:
Nuia. Tenda. Fanikiwa (Aspire. Action. Attain)
Tembelea tovuti yetu www.mustleadgroup.com